UWEKEZAJI WA NCHI YA CHINA AFRIKA
Nchi ya china imewekeza katika sekta mbalimbali Afrika,
ambapo imewekeza katika sehemu zifuatazo:
1/MIUNDOMBINU
Hapa imewekeza katika ujenzi wa barabara,viwanja vya
ndege,bandari,hospitali pamoja na shule
2/BIASHARA
Nchi ya ya china imekuwa ikifanya biashara ya kuuza,simu za
mkononi,luninga,radio,nguo pamoja na viatu ambapo vitu hivi vimekuwa vikkuuzwa
kwa bei rahisi kuliko biashara kutoka makampuni mengine ya ndani na nje ya
nchi.
3/KILIMO
Halikadhalika pia wamewekeza katika kilimo ili kupata malighafi
ya kutengenezea bidhaa zao kama vile pamba
.
4/MADINI
Hii ndio sekta ambayo wamewekeza zaidi kwasababu wanatumia madini zaidi katika
utengenezaji wa bidhaa zao kama vile simu za mkononi ambapo wanachukua madini
mengi zaidi kutoka nchi ya Zimbabwe, Zambia na Afrika kusini.
AFRIKA
WANAFAIDIKA NINI?
FAIDA
Kwaupande mwingine kuna faida lakini pia kuna hasara,
Nikianza na faida katika upande wa miundombinu kama barabara nk, Afrika inafaidika kwasababu
barabara au bandari ambazo wanajenga
wachina ziko katika ubora unaotakiwa.
Nchi ya china imekuwa ikijenga shule,kuchimba visima pamoja
nakutoa madawati,lakini pia wa Afrika wengi wamekuwa wakipata nafasi ya kusoma
katika nchi ya china.
Pia china imekuwa ikileta madaktari Afrika aidha kwaajili ya
kufanya mafunzo au kuajiriwa katika nchi za Afrika.
Waafrika wamekuwa wkifaidika na bidhaa zao kwasababu
zinauzwa kwa bei rahisi kuliko bidhaa ambazo zinauzwa ndani ya nchi kama vile
nguo na simu.
HASARA
Afrika wamekuwa wakipata hasara hasa katika viwanda
kwasababu waafrika wanapenda vitu vya bei rahisi kwahiyo wanakimbilia kununua
bidhaa za kichina kwasababu vinauzwa kwa
bei rahisi na kuacha vya kiafrika kwasababu ni ghali.
Lakini pia waafrika wamekuwa wakipata hasara kwasababu
wanapenda vitu vya bei rahisi lakini havidumu kama vile simu.
No comments:
Post a Comment